Wote tunapenda kujisikia vizuri! Tunataka kujisikia kuwa na raha, wenye nguvu na siyo wasiwasi. Hivyo tunaweza tukifikiri kuwa dawa za kulevya, pombe na sigara zitatupa hali hizo. Chunga sana! Usijidanganye! Kutumia vitu hivyo ili kupata furaha ni hatari kwani unaweza kujikuta umetopea ulevini! Kujinasua kutoka kwenye hali hiyo si lelemama! Inahitaji moyo na kujizatiti kweli kweli! Jua athari za dawa za kulevya na wapi pa kwenda kwa msaada ili ubadilike hapa.
Aina za Madawa Fahamu aina ya dawa za kulevya zitumiwazo zaidi nchini.
Athari Dawa hizi hudhuru akili na mwili na husababisha mtumiaji kuzitegemea. Huleta matatizo ya kisaikolojia, kijamii, ugumba nk. Zifahamu ili ukae mbali nazo!
Zaidi Mambo mengine mengi tu ya kufahamu kuhusu dawa za kulevya
Niende wapi Sehemu ambazo unaweza kwenda kupata msaada ikiwa umeathirika au unamfahamu aliyeathirika na dawa za kulevya zimeorodheshwa.
Maswali na Majibu Pata majibu ya maswali yaulizwayo kila mara kuhusiana na dawa za kulevya na athari zake hapa.
Stori yangu Sikiliza habari za kweli kutoka kwa watu waliotumia dawa za kulevya, walivyoathirika na walivyobadilika.
No comments:
Post a Comment