Unaanza nae vizuri ukidhani atakufaa hapo mbeleni lakini mh!.




Siku zinapozidi kwenda mbele unaona kamba inavutika zaidi upande mmoja:
  1. baada ya siku tatu tu za mahusiano yenu alikuomba umnunulie simu. simu aliyokuwa nayo anaifunga kwa "mipira kama ile ya kufungia hela" betrii inachomoka kila wakati, haina network, ya rangi ya siliver lakini imefuba balaa!,. Unaona ni muhimu kumnunulia simu lakini anasema umpe tu hiyo hela ataongezea apate nzuri zaidi, Lakini unapokutana nae kesho yake una unaona aina ya simu aliyonunua haina hadhi ya thamani ya pesa uliyompa.
  2. Pengine anakutumia sms kukuomba umtumie vocha ili mpate pia kuwasiliana
  3. ukiwa una uhakika kabisa kuwa vocha ya dola 10, lakini wewe hakupigii kamwe, ataishia "kukubip". Ukiuliza "why"...anajibu eti iliishia kumpigia mama yake!.
  4. Anafanya kazi, lakini kila mkikutana akitana kuongeza na mtu anataka kutumia simu yako tu ya kwake anasema haina credit.
  5. ukimwitaji aje kwako angalau kwa "tendo" anakuja kwa taxi, unalipa, mtakula, kumnywa, ila ukimgusa tu anakuambia "nipo katika siku zangu au sijisikii vizuri"..
  6. atataka mtoke kwenda kwenye starehe (club), ataomba hela ya kwenda saloon,ataomba ya taxi nk..
  7. Ukiwa club utalipa kiiingilio, vinywaji na kila zaga zaga mpaka siku iishe. Ukisema huna kitu atanuna na kuona unambania tu. Furaha itaishia hapo, mtakorofishana na ataondoka pasipo hata kuaga.
  8. Siku ambayo wewe upo "bize" yeye kwake anaona unamkimbia, ukimpigia simu hapike, au pengine kakuzimia kabisa.... Ukisema uende kwake hayupo, unaambiwa katoka na wenzake.
  9. Siku akikuomba umsindikize sehemu akanunue kitu, atachagua na kuelekeza wewe ndio ulipe....
  10. Ikiwa yakaribia sikukuu, anataka mwende "shopping",ukimchagulia kile ambacho wewe unaona atapendeza, anakumbia yeye hawezi kuvaa hilo "lapu lapu" atachukua ile ambayo kuilipia huwezi kutoka bila maumivu...ukikataa, kesho yake utaona kaivaa hiyo hiyo hujui alinunua saa ngapi!.
  11. Pengine atakuja na simulizi za shida kibao za kwao, utamwonea huruma umsaidie..lakini ukimweleza leo huna kitu kwa kuwa umetuma kiasi kwa mzazi wako unaona sura yake inabadilia, hanakuwa hana furaha kabisa....
Pengine unaona ni heri ya kutafuta changudoa tu, una malizana nae hata kama ni gharama kubwa inaeleweka yupo kibiashara na utakuwa mwangalifu zaidi kuliko sehemu unayojiamini kuwa kuna penzi na inafika wakati ukajikuta unajeruhiwa wewe tuuu na kuumizwa moyo!.