congrats brother.
| Stars yaichanganya Morocco | Send to a friend |
| WAKATI Kamati ya Operesheni Ushindi ya Taifa Stars chini ya mwenyekiti wake Mohamed Dewji inatarajiwa kukutana mara baada ya sikukuu ya Idd, hali ya wasiwasi imeikumba timu ya taifa ya Morocco mwezi moja kabla ya mechi yao ya ugenini dhidi ya Tanzania. Akizungumza jijini jana, Dewji alisema mikakati iliyopo ni kuhakikisha Stars inashinda mechi zake zote za nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu mashindano hayo."Tutafanya kila aina ya jitihada kuhakikisha Stars inapata pointi zote tisa za nyumbani na haipotezi mechi yoyote ya ugenini, kwa sasa kamati yangu itakaa kupanga mikakati mbali mbali ya kuhakikisha inaiua Morocco,"alisema Dewji. Alisema mikakati watakayopanga ni kuhakikisha timu inakuwa kwenye mazingira mazuri na kupata huduma zote zinazostahili, kuwaandaa wachezaji kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kuwapa motisha. "Kuandaa timu ni gharama kubwa, tutakutana baada ya sikukuu hii ya Idd kuangalia jinsi ya kubeba gharama za kuhudumia timu, kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kufanikisha Stars inashinda mechi zake zote na kufuzu,"alisema Dewji. "Mechi ya Algeria tulionewa sana, hakuna mtu ambaye alitazama mechi ile atapingana na mimi, tutapanga pia mikakati ya kuhakikisha timu yetu haionewi, na tutaipigania hadi tone la mwisho..., Licha ya kuonewa, lakini matokeo tuliyopata yamedhihirisha ukomavu wa timu yetu katika soka, ni wazi wachezaji wetu walienda wakiwa wameandaliwa kiakili ili kukabiliana vilivyo na hali ya uonevu." Stars ilipata sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Algeria kitendo ambacho kiliwaduwaza mashabiki na benchi zima la ufundi la Algeria na kupelekea kocha wao Rabah Saadane kujiuzulu. Kutokana na hali hiyo ya kocha wa Algeria kujiuzulu na Morocco kuanza mechi yake kwa suluhu walipocheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati , mashabiki wa soka wa Morocco wameingiwa wasiwasi na kusababisha kocha wa muda wa Morocco, Dominique Cuperly kuwataka mashabiki wake kuondoa hofu na kwamba Simba wa Atlas watasonga mbele. Mfaransa huyo alilimbia gazeti la Le Matin kuwa japokuwa anachukua mzigo wote wa matokeo ya suluhu ya Simba hao dhidi ya Afrika ya Kati, wananchi wa Morocco ni lazima wawe watulivu na waiunge mkono nchi yao katika kipindi chote cha michezo hiyo ya kufuzu kwa fainali za 2012. “Tunatakiwa kuangalia mbele kwa ushirikiano wa pamoja kwa sababu tutakuwa ugenini kucheza na Tanzania, nimechukua jukumu lote la matokeo dhidi ya Jamhuri y a Afrika ya Kati. "Nimesoma mengi kutoka kwenye vyombo vya habari wakitulaumu, lakini wanatakiwa kuangalia kwa makini hali yetu ya sasa,” alifafanua. “Tunahitaji muda wa kujenga upya timu ya ushindani huku tukitilia mkazo kwamba tayari tumeshaanza kampeni ya kufuzu kwa AFCON 2012, Timu haiwezi kujengwa kwa siku moja, hususani ukizingatia kwamba wachezaji hawa hawajacheza pamoja kwa miezi mingi.” Cuperly aliongeza kuwa Morocco ina wachezaji wazuri ambao wana uwezo wa kutengeneza timu bora, lakini wanahitaji benchi la ufundi bora na kuwachanganya wachezaji wengine kama Mehdi Carcela, ambao wameonyesha moyo wa kutaka kuitumikia nchi yao. “Tumeongea naye na wachezaji wengine waliosema wanataka kuichezea Morocco, kwa sasa tunaimarisha benchi la ufundi zaidi na kuhakikisha tunapata mtu bora,” alisema mtu pekee anayesubiliwa kuwasili ni Eric Gerets. |
| Send to a friend |
| KWA wakulima wa zao la muhogo wa mikoa ya kusini hususan Mtwara, wanaelewa fika habari ya matumizi mbalimbali ya zao hilo ukiacha kuchemsha, kutafuna au kukaanga kwa ajili ya mlo. Wanaelewa kwamba muhogo si chakula cha kujikimu njaa pekee, bali ni zao linaloweza kutumika kutengeneza bidhaa nyingine za viwandani kama vile biskuti, chips, keki, gundi na mkate. Huko, kuna mradi unaendelea wa kuongeza thamani ya muhogo unaojulikana kama Cava ambao tayari umeshatoa elimu kwa wasindikaji na waokaji juu ya namna ya kutumia unga wa muhogo kutengeneza bidhaa hizo. Unga wake unachanganywa kwa kiwango fulani na ngano katika kutrengenezea bidhaa hizo Taasisi ya Chakula na Lishe, imewahi kukaririwa ikisema kwamba Tanzania inaweza kuokoa kiasi cha dola za Marekani 12 hadi 24 milioni kwa mwaka ikiwa itapunguza uagizaji na matumizi ya ngano kutoka nje kwa asilimia 20 kwa mwaka... “Ikiwa wakulima wa muhogo nchini watafikia kiwango cha kuzalisha tani 300,000 hadi 600,000 za muhogo mbichi, ambao utasagwa na kupata tani 73,000 hadi 146,000 kwa mwaka.” Mmoja wa waokaji mkoani Mtwara, Mussa Hamisi anasema: “Tunachanganya unga wa muhogo na wa ngano kutengeneza mikate… kwa kweli mikate inayotoka ni mizuri sawa na ile ya ngano tupu… kwa kutumia tekenolojia hii muhogo utapata soko kwani tayari matumizi yake yameongezeka tofauti na awali ambako ulikuwa unatumiwa kwa ugali na kutafuna mbichi.” Wakulima wa Mkuranga wamepiga hatua kubwa zaidi. Wameanza kujifunza uokaji wa bidhaa hizo kwa kutumia unga wa muhogo peke yake bila ya kuchanganya na ngano. Mbali ya kutengeneza keki, wakulima hao wanatengeneza mandazi na tambi za muhogo ambazo wanasema zimeanza kupata umaarufu mkubwa kulinganisha na zile za ngano. Asia Omar Nyakilungi na Salma Ali wa Kitongoji cha Mikwasu, Kijiji cha Njopeka Mkuranga wanasema tangu walipopata ujuzi huo wa kupika keki na mandazi kwa kutumia unga wa muhogo wamekuwa wakijipatia kipato kila siku na pia kupunguza matumuzi ya vitafunwa. Nyakilungi anasema amekuwa akipika keki kwa kutumia kilo mbili za unga wa muhogo ambazo zimekuwa zikimhakikishia kipato cha Sh4,000 kila siku... "Nasomesha wanangu kwa kuuza keki hizi pamoja na shughuli nyingine na nina uhakika wa kupata mahitaji madogo madogo ya muhimu." Kwa upande wake, Salma anasema siku hizi halazimiki kununua vitafunwa kila siku asubuhi au kuchemsha muhogo kwa ajili ya chai kwani mandazi na keki anazopita mbali ya kumwingizia kipato, ndizo anazotumia kwa ajili ya kifungua kinywa. Anasema keki hiyo ina virutubisho vyote muhimu kwani huchanganywa na siagi, mayai, maziwa na sugari. Keki hiyo huwa na rangi ya kahawia." Hata hivyo, Nyakilungi anasema soko la bidhaa zao halijawa kubwa vya kutosha kwani tegemeo lao kubwa ni kuuza katika shule ya kijiji chao na zinapokuwa zimefungwa hulazimika kusimamisha biashara hiyo au kuuza kwa kiwango cha chini mno ambacho anasema hakilipi. "Hii ni changamoto kubwa kwani biashara inasimama wakati inapokuwa inahitajika zaidi. Hiki ni kipindi ambacho tunatafuta fedha kwa ajili ya ada na mahitaji mengine ya watoto wetu shuleni na ndicho ambacho hatufanyi biashara." "Naiomba Serikali itusaidie tupate mitaji ili tupanue soko letu na kuwa na uhakika wa kipato kwani tunaamini kwamba keki za muhogo pamoja na mandazi na tambi, vitakuwa na wateja wengi kutokana na ubora wake." Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Veco la Ubelgiji likishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), limeanzisha programu maalumu ya kuwasaidia wakulima wadogo wa kata sita za wilaya hiyo ili waongeze uzalishaji na kujipatia kipato kutokana na zao hilo. Ofisa Biashara na Ujenzi wa shirika hilo, Clarence Chitemi anasema programu hiyo ya miaka sita iliyoanza mwaka 2008 imelenga kutoa elimu ya kilimo bora, usindikaji wa zao hilo na masoko. "Kuna dalili njema za mafanikio. Wakulima hivi sasa wamebadilika, wamejua mbinu mbalimbali za kuandaa shamba mpaka kusindika. Tumekuwa tukiwekeza Sh 500 milioni kila mwaka tangu tulipoanza na matarajio yetu ni kuona wakulima wanakifanya kilimo cha muhogo kuwa cha kibiashara zaidi badala ya kujikimu na njaa." Mbali ya kupika bidhaa hizo, wakulima wanaonufaika na programu hiyo wamekuwa wakinufaika kwa elimu ya kuongeza uzalishaji na usindikaji kwani hivi sasa inachukua muda wa kati ya saa nne hadi sita kuvuna muhogo hadi kupata unga ambao ni mweupe kama ilivyo ule wa ngano ambao huuza kwa wastani wa Sh800 kwa kilo. Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa halmashauri hiyo, Costantine Mboya anasema muhogo ndiyo zao kuu la chakula wilayani humo likilimwa hekta 50,000 na kuzalisha tani 260,000 kwa mwaka, kiwango ambacho anasema ni kidogo kutokana na wakulima wengi kutozingatia kanuni za kilimo bora na matumizi ya zana duni. Anasema elimu wanayotoa chini ya mpango huo, inalenga kuwajengea uwezo wakulima wa kuvuna muhogo shambani na kuusindika hivyo kuuhifadhi kwa muda mrefu bila ya kuharibika. Mtaalamu wa zao la Muhogo katika Wilaya ya Mkurunga, Dereck Samwel anasema katika siku za karibuni, uzalishaji umeongezeka na kufikia tani nane na kwamba lengo ni kufikia 10 hasa ikizingatiwa kwamba kitaalamu, eka moja inapaswa kuzalisha tani 10 mpaka 15. |
EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973
Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969
Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960
EMPLOYMENT HISTORY
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992-1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985-1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982-1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982-1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977-1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977-1991
POLITICAL EXPERIENCE
CHADEMA Principal Secretary 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 To date
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch (Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
Retrieved on 13/7/2006 - www.parliament.go.tz
www.bongonewhabari.webs.comUnaanza nae vizuri ukidhani atakufaa hapo mbeleni lakini mh!.
Siku zinapozidi kwenda mbele unaona kamba inavutika zaidi upande mmoja:Pengine unaona ni heri ya kutafuta changudoa tu, una malizana nae hata kama ni gharama kubwa inaeleweka yupo kibiashara na utakuwa mwangalifu zaidi kuliko sehemu unayojiamini kuwa kuna penzi na inafika wakati ukajikuta unajeruhiwa wewe tuuu na kuumizwa moyo!.
- baada ya siku tatu tu za mahusiano yenu alikuomba umnunulie simu. simu aliyokuwa nayo anaifunga kwa "mipira kama ile ya kufungia hela" betrii inachomoka kila wakati, haina network, ya rangi ya siliver lakini imefuba balaa!,. Unaona ni muhimu kumnunulia simu lakini anasema umpe tu hiyo hela ataongezea apate nzuri zaidi, Lakini unapokutana nae kesho yake una unaona aina ya simu aliyonunua haina hadhi ya thamani ya pesa uliyompa.
- Pengine anakutumia sms kukuomba umtumie vocha ili mpate pia kuwasiliana
- ukiwa una uhakika kabisa kuwa vocha ya dola 10, lakini wewe hakupigii kamwe, ataishia "kukubip". Ukiuliza "why"...anajibu eti iliishia kumpigia mama yake!.
- Anafanya kazi, lakini kila mkikutana akitana kuongeza na mtu anataka kutumia simu yako tu ya kwake anasema haina credit.
- ukimwitaji aje kwako angalau kwa "tendo" anakuja kwa taxi, unalipa, mtakula, kumnywa, ila ukimgusa tu anakuambia "nipo katika siku zangu au sijisikii vizuri"..
- atataka mtoke kwenda kwenye starehe (club), ataomba hela ya kwenda saloon,ataomba ya taxi nk..
- Ukiwa club utalipa kiiingilio, vinywaji na kila zaga zaga mpaka siku iishe. Ukisema huna kitu atanuna na kuona unambania tu. Furaha itaishia hapo, mtakorofishana na ataondoka pasipo hata kuaga.
- Siku ambayo wewe upo "bize" yeye kwake anaona unamkimbia, ukimpigia simu hapike, au pengine kakuzimia kabisa.... Ukisema uende kwake hayupo, unaambiwa katoka na wenzake.
- Siku akikuomba umsindikize sehemu akanunue kitu, atachagua na kuelekeza wewe ndio ulipe....
- Ikiwa yakaribia sikukuu, anataka mwende "shopping",ukimchagulia kile ambacho wewe unaona atapendeza, anakumbia yeye hawezi kuvaa hilo "lapu lapu" atachukua ile ambayo kuilipia huwezi kutoka bila maumivu...ukikataa, kesho yake utaona kaivaa hiyo hiyo hujui alinunua saa ngapi!.
- Pengine atakuja na simulizi za shida kibao za kwao, utamwonea huruma umsaidie..lakini ukimweleza leo huna kitu kwa kuwa umetuma kiasi kwa mzazi wako unaona sura yake inabadilia, hanakuwa hana furaha kabisa....
"Life is not measured by the breaths we take, but by the moments that take our breath away, Keep smiling, it makes people wonder what you're up to."





Yaliyomo[ficha] |
| Send to a friend |
| Richard Kihiyo MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watumiaji wa simu za mikononi kupuuza ujumbe wa tahadhari ulioanza kusambazwa jana na watu wasiojulikana, ikisema kuwa ni uzushi. Jana kulikuwa na aina mbili za taarifa za tahadhari zilizokuwa zikitumwa kwa wateja wa simu za mikononi. Ujumbe wa kwanza unasema: “Ukipigiwa simu kwa private no (namba binafsi). au ikiandika call kwa red colour (rangi nyekundu) usipokee, ni mionzi, utapalarize (utapooza) na kufa. Imetokea Kenya watu wamekufa. Julisha ndugu na jamaa wote.” Ujumbe mwingine unawataka watumiaji wa huduma hiyo wasipokee simu yoyote watakayopigiwa kupitia namba 7888308001, 9316048121, 9876266211, 9888854137 na 9876715587. Ujumbe huo unasema: "Namba hii inapigwa na rangi nyekundu, unaweza kupata brain damage (tatizo la ubongo) kwa kupokea simu. Watu 27 walifariki mara tuu baada ya kupokea simu iliyopigwa kutoka katika namba hizo." Ujumbe huo ulisababisha watumiaji wa simu kuingiwa na wasiwasi na baadhi waliwasiliana na chumba cha habari cha Mwananchi Communications kutaka ufafanuzi wa suala hilo na wengine wakieleza hofu ya kupooza. Hata hivyo, taarifa iliyotumwa na msemaji wa TCRA, Innocent Mungy ambayo imesainiwa na kurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkhoma, inasema: “Ujumbe huo unatakiwa kupuuzwa kwa kuwa ni uzushi usuokuwa na ukweli wowote.” Kutokana na ujumbe huo kusambazwa kwa watu wengi, TCRA imesema hakuna ukweli na hivyo kuwataka wananchi kuupuuzia. "Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote," inasema taarifa hiyo ya TCRA. Ilifafanua kuwa kutokanha na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu mbalimbali duniani ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. TCRA iliwataka wote kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta ambazo zinatumiwa ulimwenguni kote bila madhara yoyote. "Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema," inasema sheemu ya taarifa hiyo. Mmoja wa watumiaji wa simu za mkononi, Frank Kimboyi ambaye naye alitumiwa ujumbe huo, alisema mwanzoni alipata wasiwasi mkubwa. "Baada ya kuupokea kidogo nilishituka, lakini baada ya kukaa na kutafakari uwezekano wa kitu kama hicho kutokea niliona ni mdogo na nikaamua kuupuuzia," alisema Kimboyi. |