BONGO NEWS
Sunday, September 19, 2010
nothern highlands form four graduation
masela wakiphotoana kabla ya ngoma yenyewe kuanza its true dat was theeir day congrats brother.Mwalimu iwambo na wanafunzi wake
Friday, September 10, 2010
Stars yaichanganya Morocco
Stars yaichanganya Morocco | Send to a friend |
WAKATI Kamati ya Operesheni Ushindi ya Taifa Stars chini ya mwenyekiti wake Mohamed Dewji inatarajiwa kukutana mara baada ya sikukuu ya Idd, hali ya wasiwasi imeikumba timu ya taifa ya Morocco mwezi moja kabla ya mechi yao ya ugenini dhidi ya Tanzania. Akizungumza jijini jana, Dewji alisema mikakati iliyopo ni kuhakikisha Stars inashinda mechi zake zote za nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu mashindano hayo."Tutafanya kila aina ya jitihada kuhakikisha Stars inapata pointi zote tisa za nyumbani na haipotezi mechi yoyote ya ugenini, kwa sasa kamati yangu itakaa kupanga mikakati mbali mbali ya kuhakikisha inaiua Morocco,"alisema Dewji. Alisema mikakati watakayopanga ni kuhakikisha timu inakuwa kwenye mazingira mazuri na kupata huduma zote zinazostahili, kuwaandaa wachezaji kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kuwapa motisha. "Kuandaa timu ni gharama kubwa, tutakutana baada ya sikukuu hii ya Idd kuangalia jinsi ya kubeba gharama za kuhudumia timu, kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kufanikisha Stars inashinda mechi zake zote na kufuzu,"alisema Dewji. "Mechi ya Algeria tulionewa sana, hakuna mtu ambaye alitazama mechi ile atapingana na mimi, tutapanga pia mikakati ya kuhakikisha timu yetu haionewi, na tutaipigania hadi tone la mwisho..., Licha ya kuonewa, lakini matokeo tuliyopata yamedhihirisha ukomavu wa timu yetu katika soka, ni wazi wachezaji wetu walienda wakiwa wameandaliwa kiakili ili kukabiliana vilivyo na hali ya uonevu." Stars ilipata sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Algeria kitendo ambacho kiliwaduwaza mashabiki na benchi zima la ufundi la Algeria na kupelekea kocha wao Rabah Saadane kujiuzulu. Kutokana na hali hiyo ya kocha wa Algeria kujiuzulu na Morocco kuanza mechi yake kwa suluhu walipocheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati , mashabiki wa soka wa Morocco wameingiwa wasiwasi na kusababisha kocha wa muda wa Morocco, Dominique Cuperly kuwataka mashabiki wake kuondoa hofu na kwamba Simba wa Atlas watasonga mbele. Mfaransa huyo alilimbia gazeti la Le Matin kuwa japokuwa anachukua mzigo wote wa matokeo ya suluhu ya Simba hao dhidi ya Afrika ya Kati, wananchi wa Morocco ni lazima wawe watulivu na waiunge mkono nchi yao katika kipindi chote cha michezo hiyo ya kufuzu kwa fainali za 2012. “Tunatakiwa kuangalia mbele kwa ushirikiano wa pamoja kwa sababu tutakuwa ugenini kucheza na Tanzania, nimechukua jukumu lote la matokeo dhidi ya Jamhuri y a Afrika ya Kati. "Nimesoma mengi kutoka kwenye vyombo vya habari wakitulaumu, lakini wanatakiwa kuangalia kwa makini hali yetu ya sasa,” alifafanua. “Tunahitaji muda wa kujenga upya timu ya ushindani huku tukitilia mkazo kwamba tayari tumeshaanza kampeni ya kufuzu kwa AFCON 2012, Timu haiwezi kujengwa kwa siku moja, hususani ukizingatia kwamba wachezaji hawa hawajacheza pamoja kwa miezi mingi.” Cuperly aliongeza kuwa Morocco ina wachezaji wazuri ambao wana uwezo wa kutengeneza timu bora, lakini wanahitaji benchi la ufundi bora na kuwachanganya wachezaji wengine kama Mehdi Carcela, ambao wameonyesha moyo wa kutaka kuitumikia nchi yao. “Tumeongea naye na wachezaji wengine waliosema wanataka kuichezea Morocco, kwa sasa tunaimarisha benchi la ufundi zaidi na kuhakikisha tunapata mtu bora,” alisema mtu pekee anayesubiliwa kuwasili ni Eric Gerets. |
Umewahi kuonja keki na tambi za muhogo?
Send to a friend |
Na Rashid Kejo KWA wakulima wa zao la muhogo wa mikoa ya kusini hususan Mtwara, wanaelewa fika habari ya matumizi mbalimbali ya zao hilo ukiacha kuchemsha, kutafuna au kukaanga kwa ajili ya mlo. Wanaelewa kwamba muhogo si chakula cha kujikimu njaa pekee, bali ni zao linaloweza kutumika kutengeneza bidhaa nyingine za viwandani kama vile biskuti, chips, keki, gundi na mkate. Huko, kuna mradi unaendelea wa kuongeza thamani ya muhogo unaojulikana kama Cava ambao tayari umeshatoa elimu kwa wasindikaji na waokaji juu ya namna ya kutumia unga wa muhogo kutengeneza bidhaa hizo. Unga wake unachanganywa kwa kiwango fulani na ngano katika kutrengenezea bidhaa hizo Taasisi ya Chakula na Lishe, imewahi kukaririwa ikisema kwamba Tanzania inaweza kuokoa kiasi cha dola za Marekani 12 hadi 24 milioni kwa mwaka ikiwa itapunguza uagizaji na matumizi ya ngano kutoka nje kwa asilimia 20 kwa mwaka... “Ikiwa wakulima wa muhogo nchini watafikia kiwango cha kuzalisha tani 300,000 hadi 600,000 za muhogo mbichi, ambao utasagwa na kupata tani 73,000 hadi 146,000 kwa mwaka.” Mmoja wa waokaji mkoani Mtwara, Mussa Hamisi anasema: “Tunachanganya unga wa muhogo na wa ngano kutengeneza mikate… kwa kweli mikate inayotoka ni mizuri sawa na ile ya ngano tupu… kwa kutumia tekenolojia hii muhogo utapata soko kwani tayari matumizi yake yameongezeka tofauti na awali ambako ulikuwa unatumiwa kwa ugali na kutafuna mbichi.” Wakulima wa Mkuranga wamepiga hatua kubwa zaidi. Wameanza kujifunza uokaji wa bidhaa hizo kwa kutumia unga wa muhogo peke yake bila ya kuchanganya na ngano. Mbali ya kutengeneza keki, wakulima hao wanatengeneza mandazi na tambi za muhogo ambazo wanasema zimeanza kupata umaarufu mkubwa kulinganisha na zile za ngano. Asia Omar Nyakilungi na Salma Ali wa Kitongoji cha Mikwasu, Kijiji cha Njopeka Mkuranga wanasema tangu walipopata ujuzi huo wa kupika keki na mandazi kwa kutumia unga wa muhogo wamekuwa wakijipatia kipato kila siku na pia kupunguza matumuzi ya vitafunwa. Nyakilungi anasema amekuwa akipika keki kwa kutumia kilo mbili za unga wa muhogo ambazo zimekuwa zikimhakikishia kipato cha Sh4,000 kila siku... "Nasomesha wanangu kwa kuuza keki hizi pamoja na shughuli nyingine na nina uhakika wa kupata mahitaji madogo madogo ya muhimu." Kwa upande wake, Salma anasema siku hizi halazimiki kununua vitafunwa kila siku asubuhi au kuchemsha muhogo kwa ajili ya chai kwani mandazi na keki anazopita mbali ya kumwingizia kipato, ndizo anazotumia kwa ajili ya kifungua kinywa. Anasema keki hiyo ina virutubisho vyote muhimu kwani huchanganywa na siagi, mayai, maziwa na sugari. Keki hiyo huwa na rangi ya kahawia." Hata hivyo, Nyakilungi anasema soko la bidhaa zao halijawa kubwa vya kutosha kwani tegemeo lao kubwa ni kuuza katika shule ya kijiji chao na zinapokuwa zimefungwa hulazimika kusimamisha biashara hiyo au kuuza kwa kiwango cha chini mno ambacho anasema hakilipi. "Hii ni changamoto kubwa kwani biashara inasimama wakati inapokuwa inahitajika zaidi. Hiki ni kipindi ambacho tunatafuta fedha kwa ajili ya ada na mahitaji mengine ya watoto wetu shuleni na ndicho ambacho hatufanyi biashara." "Naiomba Serikali itusaidie tupate mitaji ili tupanue soko letu na kuwa na uhakika wa kipato kwani tunaamini kwamba keki za muhogo pamoja na mandazi na tambi, vitakuwa na wateja wengi kutokana na ubora wake." Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Veco la Ubelgiji likishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), limeanzisha programu maalumu ya kuwasaidia wakulima wadogo wa kata sita za wilaya hiyo ili waongeze uzalishaji na kujipatia kipato kutokana na zao hilo. Ofisa Biashara na Ujenzi wa shirika hilo, Clarence Chitemi anasema programu hiyo ya miaka sita iliyoanza mwaka 2008 imelenga kutoa elimu ya kilimo bora, usindikaji wa zao hilo na masoko. "Kuna dalili njema za mafanikio. Wakulima hivi sasa wamebadilika, wamejua mbinu mbalimbali za kuandaa shamba mpaka kusindika. Tumekuwa tukiwekeza Sh 500 milioni kila mwaka tangu tulipoanza na matarajio yetu ni kuona wakulima wanakifanya kilimo cha muhogo kuwa cha kibiashara zaidi badala ya kujikimu na njaa." Mbali ya kupika bidhaa hizo, wakulima wanaonufaika na programu hiyo wamekuwa wakinufaika kwa elimu ya kuongeza uzalishaji na usindikaji kwani hivi sasa inachukua muda wa kati ya saa nne hadi sita kuvuna muhogo hadi kupata unga ambao ni mweupe kama ilivyo ule wa ngano ambao huuza kwa wastani wa Sh800 kwa kilo. Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa halmashauri hiyo, Costantine Mboya anasema muhogo ndiyo zao kuu la chakula wilayani humo likilimwa hekta 50,000 na kuzalisha tani 260,000 kwa mwaka, kiwango ambacho anasema ni kidogo kutokana na wakulima wengi kutozingatia kanuni za kilimo bora na matumizi ya zana duni. Anasema elimu wanayotoa chini ya mpango huo, inalenga kuwajengea uwezo wakulima wa kuvuna muhogo shambani na kuusindika hivyo kuuhifadhi kwa muda mrefu bila ya kuharibika. Mtaalamu wa zao la Muhogo katika Wilaya ya Mkurunga, Dereck Samwel anasema katika siku za karibuni, uzalishaji umeongezeka na kufikia tani nane na kwamba lengo ni kufikia 10 hasa ikizingatiwa kwamba kitaalamu, eka moja inapaswa kuzalisha tani 10 mpaka 15. |
Sunday, September 5, 2010
Tuesday, June 30, 2009
Fresh Start
I've been blogging on blogspot ever since I was 17, being highly bored during my two week break in between my SPM exams.
And it's been 5 years ever since!
Well, I guess I just wanted a fresh look and so I am now moving to a new page :
www.eemay101.wordpress.com
I hope you'll continue to enjoy snippets of the nonsensical things Lee Ee May finds herself doing in life.
=)
Posted by Ee May at 12:07 AM 18 comments
Wednesday, June 24, 2009
EeMay likes...
Fresh Start
I've been blogging on blogspot ever since I was 17, being highly bored during my two week break in between my SPM exams.
And it's been 5 years ever since!
Well, I guess I just wanted a fresh look and so I am now moving to a new page :
www.eemay101.wordpress.com
I hope you'll continue to enjoy snippets of the nonsensical things Lee Ee May finds herself doing in life.
=)
Posted by Ee May at 12:07 AM 18 comments
Wednesday, June 24, 2009
EeMay likes...
Hii ni CV ya Dr Slaa
EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973
Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969
Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960
EMPLOYMENT HISTORY
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992-1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985-1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982-1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982-1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977-1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977-1991
POLITICAL EXPERIENCE
CHADEMA Principal Secretary 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 To date
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch (Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
Retrieved on 13/7/2006 - www.parliament.go.tz
Saturday, September 4, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)