Friday, September 10, 2010

Stars yaichanganya Morocco

Stars yaichanganya Morocco  Send to a friend

Mwenyekiti wa Kamati ya Operesheni Ushindi ya Taifa Stars,Mohamed Dewji
Vicky Kimaro
WAKATI Kamati ya Operesheni Ushindi ya Taifa Stars chini ya mwenyekiti wake Mohamed Dewji inatarajiwa kukutana mara baada ya sikukuu ya Idd, hali ya wasiwasi imeikumba timu ya taifa ya Morocco mwezi moja kabla ya mechi yao ya ugenini dhidi ya Tanzania.

Akizungumza jijini jana, Dewji alisema mikakati iliyopo ni kuhakikisha Stars inashinda mechi zake zote za nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu mashindano hayo."Tutafanya kila aina ya jitihada kuhakikisha Stars inapata pointi zote tisa za nyumbani na haipotezi mechi yoyote ya ugenini, kwa sasa kamati yangu itakaa kupanga mikakati mbali mbali ya kuhakikisha inaiua Morocco,"alisema Dewji.

Alisema mikakati watakayopanga ni kuhakikisha timu inakuwa kwenye mazingira mazuri na kupata huduma zote zinazostahili, kuwaandaa wachezaji kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kuwapa motisha.

"Kuandaa timu ni gharama kubwa, tutakutana baada ya sikukuu hii ya Idd kuangalia jinsi ya kubeba gharama za kuhudumia timu, kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kufanikisha Stars inashinda mechi zake zote na kufuzu,"alisema Dewji.

"Mechi ya Algeria tulionewa sana, hakuna mtu ambaye alitazama mechi ile atapingana na mimi, tutapanga pia mikakati ya kuhakikisha timu yetu haionewi, na tutaipigania hadi tone la mwisho..., Licha ya kuonewa, lakini matokeo tuliyopata yamedhihirisha ukomavu wa timu yetu katika soka, ni wazi wachezaji wetu walienda wakiwa wameandaliwa kiakili ili kukabiliana vilivyo na hali ya uonevu."

Stars ilipata sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Algeria kitendo ambacho kiliwaduwaza mashabiki na benchi zima la ufundi la Algeria na kupelekea kocha wao Rabah Saadane kujiuzulu.

Kutokana na hali hiyo ya kocha wa Algeria kujiuzulu na Morocco kuanza mechi yake kwa suluhu walipocheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati , mashabiki wa soka wa Morocco wameingiwa wasiwasi na kusababisha kocha wa muda wa Morocco, Dominique Cuperly kuwataka mashabiki wake kuondoa hofu na kwamba Simba wa Atlas watasonga mbele.

Mfaransa huyo alilimbia gazeti la Le Matin kuwa japokuwa anachukua mzigo wote wa matokeo ya suluhu ya Simba hao dhidi ya Afrika ya Kati, wananchi wa Morocco ni lazima wawe watulivu na waiunge mkono nchi yao katika kipindi chote cha michezo hiyo ya kufuzu kwa fainali za 2012.

“Tunatakiwa kuangalia mbele kwa ushirikiano wa pamoja kwa sababu tutakuwa ugenini kucheza na Tanzania, nimechukua jukumu lote la matokeo dhidi ya Jamhuri y a Afrika ya Kati.

"Nimesoma mengi kutoka kwenye vyombo vya habari wakitulaumu, lakini wanatakiwa kuangalia kwa makini hali yetu ya sasa,” alifafanua.

“Tunahitaji muda wa kujenga upya timu ya ushindani huku tukitilia mkazo kwamba tayari tumeshaanza kampeni ya kufuzu kwa AFCON 2012, Timu haiwezi kujengwa kwa siku moja, hususani ukizingatia kwamba wachezaji hawa hawajacheza pamoja kwa miezi mingi.”

Cuperly aliongeza kuwa Morocco ina wachezaji wazuri ambao wana uwezo wa kutengeneza timu bora, lakini wanahitaji benchi la ufundi bora na kuwachanganya wachezaji wengine kama Mehdi Carcela, ambao wameonyesha moyo wa kutaka kuitumikia nchi yao.

“Tumeongea naye na wachezaji wengine waliosema wanataka kuichezea Morocco, kwa sasa tunaimarisha benchi la ufundi zaidi na kuhakikisha tunapata mtu bora,” alisema mtu pekee anayesubiliwa kuwasili ni Eric Gerets.


Umewahi kuonja keki na tambi za muhogo?

 Send to a friend



Mkate wa muhogo
Na Rashid Kejo
KWA wakulima wa zao la muhogo wa mikoa ya kusini hususan Mtwara, wanaelewa fika habari ya matumizi mbalimbali ya zao hilo ukiacha kuchemsha, kutafuna au kukaanga kwa ajili ya mlo.

Wanaelewa kwamba muhogo si chakula cha kujikimu njaa pekee, bali ni zao linaloweza kutumika kutengeneza bidhaa nyingine za viwandani kama vile biskuti, chips, keki, gundi na mkate.

Huko, kuna mradi unaendelea wa kuongeza thamani ya muhogo unaojulikana kama Cava ambao tayari umeshatoa elimu kwa wasindikaji na waokaji juu ya namna ya kutumia unga wa muhogo kutengeneza bidhaa hizo.

Unga wake unachanganywa kwa kiwango fulani na ngano katika kutrengenezea bidhaa hizo

Taasisi ya Chakula na Lishe, imewahi kukaririwa ikisema kwamba Tanzania inaweza kuokoa kiasi cha dola za Marekani 12 hadi 24 milioni kwa mwaka ikiwa itapunguza uagizaji na matumizi ya ngano kutoka nje kwa asilimia 20 kwa mwaka... “Ikiwa wakulima wa muhogo nchini watafikia kiwango cha kuzalisha tani 300,000 hadi 600,000 za muhogo mbichi, ambao utasagwa na kupata tani 73,000 hadi 146,000 kwa mwaka.”

Mmoja wa waokaji mkoani Mtwara, Mussa Hamisi anasema:
“Tunachanganya unga wa muhogo na wa ngano kutengeneza mikate… kwa kweli mikate inayotoka ni mizuri sawa na ile ya ngano tupu… kwa kutumia tekenolojia hii muhogo utapata soko kwani tayari matumizi yake yameongezeka tofauti na awali ambako ulikuwa unatumiwa kwa ugali na kutafuna mbichi.”

Wakulima wa Mkuranga wamepiga hatua kubwa zaidi. Wameanza kujifunza uokaji wa bidhaa hizo kwa kutumia unga wa muhogo peke yake bila ya kuchanganya na ngano.

Mbali ya kutengeneza keki, wakulima hao wanatengeneza mandazi na tambi za muhogo ambazo wanasema zimeanza kupata umaarufu mkubwa kulinganisha na zile za ngano.

Asia Omar Nyakilungi na Salma Ali wa Kitongoji cha Mikwasu, Kijiji cha Njopeka Mkuranga wanasema tangu walipopata ujuzi huo wa kupika keki na mandazi kwa kutumia unga wa muhogo wamekuwa wakijipatia kipato kila siku na pia kupunguza matumuzi ya vitafunwa.

Nyakilungi anasema amekuwa akipika keki kwa kutumia kilo mbili za unga wa muhogo ambazo zimekuwa zikimhakikishia kipato cha Sh4,000 kila siku... "Nasomesha wanangu kwa kuuza keki hizi pamoja na shughuli nyingine na nina uhakika wa kupata mahitaji madogo madogo ya muhimu."

Kwa upande wake, Salma anasema siku hizi halazimiki kununua vitafunwa kila siku asubuhi au kuchemsha muhogo kwa ajili ya chai kwani mandazi na keki anazopita mbali ya kumwingizia kipato, ndizo anazotumia kwa ajili ya kifungua kinywa.

Anasema keki hiyo ina virutubisho vyote muhimu kwani huchanganywa na siagi, mayai, maziwa na sugari. Keki hiyo huwa na rangi ya kahawia."

Hata hivyo, Nyakilungi anasema soko la bidhaa zao halijawa kubwa vya kutosha kwani tegemeo lao kubwa ni kuuza katika shule ya kijiji chao na zinapokuwa zimefungwa hulazimika kusimamisha biashara hiyo au kuuza kwa kiwango cha chini mno ambacho anasema hakilipi.

"Hii ni changamoto kubwa kwani biashara inasimama wakati inapokuwa inahitajika zaidi. Hiki ni kipindi ambacho tunatafuta fedha kwa ajili ya ada na mahitaji mengine ya watoto wetu shuleni na ndicho ambacho hatufanyi biashara."

"Naiomba Serikali itusaidie tupate mitaji ili tupanue soko letu na kuwa na uhakika wa kipato kwani tunaamini kwamba keki za muhogo pamoja na mandazi na tambi, vitakuwa na wateja wengi kutokana na ubora wake."

Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Veco la Ubelgiji likishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), limeanzisha programu maalumu ya kuwasaidia wakulima wadogo wa kata sita za wilaya hiyo ili waongeze uzalishaji na kujipatia kipato kutokana na zao hilo.

Ofisa Biashara na Ujenzi wa  shirika hilo, Clarence Chitemi anasema programu hiyo ya miaka sita iliyoanza mwaka 2008 imelenga kutoa elimu ya kilimo bora, usindikaji wa zao hilo na masoko.

"Kuna dalili njema za mafanikio. Wakulima hivi sasa wamebadilika, wamejua mbinu mbalimbali za kuandaa shamba mpaka kusindika. Tumekuwa tukiwekeza Sh 500 milioni kila mwaka tangu tulipoanza na matarajio yetu ni kuona wakulima wanakifanya kilimo cha muhogo kuwa cha kibiashara zaidi badala ya kujikimu na njaa."

Mbali ya kupika bidhaa hizo, wakulima wanaonufaika na programu hiyo wamekuwa wakinufaika kwa elimu ya kuongeza uzalishaji na usindikaji kwani hivi sasa inachukua muda wa kati ya saa nne hadi sita kuvuna muhogo hadi kupata unga ambao ni mweupe kama ilivyo ule wa ngano ambao huuza kwa wastani wa Sh800 kwa kilo.

Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa halmashauri hiyo, Costantine Mboya anasema muhogo ndiyo zao kuu la chakula wilayani humo likilimwa hekta 50,000 na kuzalisha tani 260,000 kwa mwaka, kiwango ambacho anasema ni kidogo kutokana na wakulima wengi kutozingatia kanuni za kilimo bora na matumizi ya zana duni.

Anasema elimu wanayotoa chini ya mpango huo, inalenga kuwajengea uwezo wakulima wa kuvuna muhogo shambani na kuusindika hivyo kuuhifadhi kwa muda mrefu bila ya kuharibika.

Mtaalamu wa zao la Muhogo katika Wilaya ya Mkurunga, Dereck Samwel anasema katika siku za karibuni, uzalishaji umeongezeka na kufikia tani nane na kwamba lengo ni kufikia 10 hasa ikizingatiwa kwamba kitaalamu, eka moja inapaswa kuzalisha tani 10 mpaka 15.

Sunday, September 5, 2010

Tuesday, June 30, 2009
Fresh Start
I've been blogging on blogspot ever since I was 17, being highly bored during my two week break in between my SPM exams.

And it's been 5 years ever since!

Well, I guess I just wanted a fresh look and so I am now moving to a new page :

www.eemay101.wordpress.com

I hope you'll continue to enjoy snippets of the nonsensical things Lee Ee May finds herself doing in life.

=)
Posted by Ee May at 12:07 AM 18 comments
Wednesday, June 24, 2009
EeMay likes...

KIBAKA


Yaani ukiwa kibaka utadhalilishwa mpaka ufe, unasachiwa mpaka kwenye mashine? HAki hakuna Afrika!!

Hii ni CV ya Dr Slaa


EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993

TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985

St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981

St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]

Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973

Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969

Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960

EMPLOYMENT HISTORY
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992-1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985-1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982-1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982-1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977-1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977-1991

POLITICAL EXPERIENCE

CHADEMA Principal Secretary 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 To date
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch (Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977

Retrieved on 13/7/2006 - www.parliament.go.tz

Saturday, September 4, 2010

HOT

WHAT Rihard'z view

www.bongonewhabari.webs.com
"Life is not measured by the breaths we take, but by the moments that take our breath away, Keep smiling, it makes people wonder what you're up to."

Afadhali changudoa


Unaanza nae vizuri ukidhani atakufaa hapo mbeleni lakini mh!.




Siku zinapozidi kwenda mbele unaona kamba inavutika zaidi upande mmoja:
  1. baada ya siku tatu tu za mahusiano yenu alikuomba umnunulie simu. simu aliyokuwa nayo anaifunga kwa "mipira kama ile ya kufungia hela" betrii inachomoka kila wakati, haina network, ya rangi ya siliver lakini imefuba balaa!,. Unaona ni muhimu kumnunulia simu lakini anasema umpe tu hiyo hela ataongezea apate nzuri zaidi, Lakini unapokutana nae kesho yake una unaona aina ya simu aliyonunua haina hadhi ya thamani ya pesa uliyompa.
  2. Pengine anakutumia sms kukuomba umtumie vocha ili mpate pia kuwasiliana
  3. ukiwa una uhakika kabisa kuwa vocha ya dola 10, lakini wewe hakupigii kamwe, ataishia "kukubip". Ukiuliza "why"...anajibu eti iliishia kumpigia mama yake!.
  4. Anafanya kazi, lakini kila mkikutana akitana kuongeza na mtu anataka kutumia simu yako tu ya kwake anasema haina credit.
  5. ukimwitaji aje kwako angalau kwa "tendo" anakuja kwa taxi, unalipa, mtakula, kumnywa, ila ukimgusa tu anakuambia "nipo katika siku zangu au sijisikii vizuri"..
  6. atataka mtoke kwenda kwenye starehe (club), ataomba hela ya kwenda saloon,ataomba ya taxi nk..
  7. Ukiwa club utalipa kiiingilio, vinywaji na kila zaga zaga mpaka siku iishe. Ukisema huna kitu atanuna na kuona unambania tu. Furaha itaishia hapo, mtakorofishana na ataondoka pasipo hata kuaga.
  8. Siku ambayo wewe upo "bize" yeye kwake anaona unamkimbia, ukimpigia simu hapike, au pengine kakuzimia kabisa.... Ukisema uende kwake hayupo, unaambiwa katoka na wenzake.
  9. Siku akikuomba umsindikize sehemu akanunue kitu, atachagua na kuelekeza wewe ndio ulipe....
  10. Ikiwa yakaribia sikukuu, anataka mwende "shopping",ukimchagulia kile ambacho wewe unaona atapendeza, anakumbia yeye hawezi kuvaa hilo "lapu lapu" atachukua ile ambayo kuilipia huwezi kutoka bila maumivu...ukikataa, kesho yake utaona kaivaa hiyo hiyo hujui alinunua saa ngapi!.
  11. Pengine atakuja na simulizi za shida kibao za kwao, utamwonea huruma umsaidie..lakini ukimweleza leo huna kitu kwa kuwa umetuma kiasi kwa mzazi wako unaona sura yake inabadilia, hanakuwa hana furaha kabisa....
Pengine unaona ni heri ya kutafuta changudoa tu, una malizana nae hata kama ni gharama kubwa inaeleweka yupo kibiashara na utakuwa mwangalifu zaidi kuliko sehemu unayojiamini kuwa kuna penzi na inafika wakati ukajikuta unajeruhiwa wewe tuuu na kuumizwa moyo!.
"Life is not measured by the breaths we take, but by the moments that take our breath away, Keep smiling, it makes people wonder what you're up to."

Pedicure - How To Foot & Nail Advice

Tuesday, January 5, 2010

Pedicure - How To Foot & Nail Advice



While planning your beauty routine, don't neglect your feet that carry your around all day long. Well-groomed and healthy feet and nails go a long way in adding to your personal style statement. Are you plagued by cracked heels or dry and tired feet? Give yourself a home pedicure or go in for a salon pedicure. Arm yourself with a pedicure kit and get going. Choose from a range of foot products, be it foot scrubs or creams or alluring nail varnish shades. A spa pedicure is a relaxing experience that will leave your feet smooth and sexy.

Foot & toe pedicure
You can give your feet some much-deserved pampering at home with a home pedicure. Alternatively you can opt for a salon pedicure where you can sit back and relax and watch your feet get a makeover. What is a pedicure all about? The basic fundamentals for any pedicure are the same - soak, smoothen, pamper and polish.

1. Cut your nails straight across with nail clippers. Use a file to smoothen the edges. Square nails with rounded edges are popular.


2. Soaking the feet in warm soapsuds is the first critical step to a good pedicure. Throw in your favorite bath salts or just a teaspoon of olive oil. You could add a cup of Epsom salt, a natural disinfectant. The warm water works wonders on the tired and hardened skin on the feet. Ensure that old nail varnish is removed prior to soaking the feet in water. Aromatic oils such as chamomile are used to soften the skin while lavender heals cuts and fissures.

3. Smoothen the dead cells off the heels with a foot scrubber or pumice stone. Use a foot file to smoothen the heels and the balls of your feet. Apply an exfoliating scrub or paste to smoothen the skin on the feet.

4. Use cuticle oil and push back cuticle and gently clean them. Use exfoliating scrubs with a nailbrush to clean the area.

5. Slather on rich moisturizing cream on the feet. Let the feet bask in the pampering massage. . Massaging feet increases blood circulation, relaxes muscles and relieves aches and pains. Don't neglect your toes. Rub between toes, using a gentle touch. Finish by rubbing each toe individually. Give both feet equal care. Massage cream is applied to the calves too.

6. Clean up all traces of oil before applying nail varnish. Create space between toes with a foam toe separator. Apply nail polish from the bottom of the nails to the tips. Applying a little polish below your nails is said to help prevent early chapping of the nail polish. Apply base coats and then two coats of color for long-lasting effect. Allow some time between coats of nail polish for better bonding. Let your polish dry for a few hours before putting on close-toed shoes.


Pedicure spa
At a pedicure spa, you can enjoy the benefits of an exotic foot treatment with a multitude of creams and foot treatments. Soak away your stress by dipping your feet in warm water filled with bath salts or sea salts. Enjoy the benefits of a mineral rich seaweed soak for your tired feet. Some spas offer marine algae and menthol soak that can heal tired feet. Let the spa professional scrub your heels and feet with a special quartz crystal scrub or a fruit based scrub. A pumice stone or foot brush is used to buff down calluses and slough away the dead skin.

Hot oil paraffin wax treatment can go a long way in smoothening rough skin leaving your feet smooth and silken. The warm paraffin wax application stimulates circulation and softens the skin. It helps relieve arthritic and other painful conditions and promotes healthy growth of nails. Your nails are trimmed and cuticles are cleaned. Envelop your feet in a masque that will soften your skin and rejuvenate it. At a spa pedicure, enjoy a therapeutic foot massage with aromatherapy oils or botanical extracts. Peppermint foot cream is a favorite on account of its healing and relaxing properties. Detox your feet and get them looking radiant and relaxed at a spa pedicure.

French pedicure
If you don't want to go in for bold bright colors on your feet, why not try a French pedicure? The main feature of a French pedicure is the clear or pearl shaded varnish that look classic and ideal for corporate wear as well as the evening out. A French pedicure works much like a regular pedicure except for the French paint on the nails. Your nails are painted with pearl or mauve colored varnish and a hint of white is applied on the top. Tips for a DIY French pedicure:


  • Follow all the routine soaking and cleansing of the feet. Soften the heels and clean up the toenails.

  • Apply sheer pink, natural or peach polish on the entire nail.

  • Apply a small strip of white polish on the tips of the toenails.

  • Apply a clear coat to seal in the color.



  • You can pick up a French pedicure kit that will provide you the colors needed for the French polish. You can show off your pearly toenails in delicate slippers or open-toed sandals.

    Foot pedicure kit
    Pick up a pedicure kit to give yourself a routine pedicure at home. Pedicure kits contain all the basic equipment required - Toenail clippers, nail file, toenail scissors, toe separators, Nail brush, foot scraper, orange stick and nail filer. You can treat yourself to Dead Sea bath salts that can rejuvenate the tired soles. Medicated bath salts help in reducing stress and relaxing feet muscles. Arm yourself with a foot cream that will reduce the dryness and prevent heels from cracking. Invest in a paraffin wax foot-bath if you are regular in your home pedicures.

    You can use it for hands, wrists, feet and elbows and smoothen the skin. Arm yourself with a good foot scrub. You can choose from peppermint and plum or flaxseed or aloe vera scrubs. Stocking up a bottle of cuticle oil can come in very handy during manicures and pedicures. Foot creams come in a wide range too - peppermint cream for stimulation and scent or tea tree cream to soothe the skin and remove traces of foot odor. Alternatively you can opt for creams with rosemary or eucalyptus. You can keep up the foot care by regularly using the pumice stone to tackle cracked heels. Use moisturizers and foot cream to minimize the effect of wear and tear on the feet.

    You can use it for hands, wrists, feet and elbows and smoothen the skin. Arm yourself with a good foot scrub. You can choose from peppermint and plum or flaxseed or aloe vera scrubs. Stocking up a bottle of cuticle oil can come in very handy during manicures and pedicures. Foot creams come in a wide range too - peppermint cream for stimulation and scent or tea tree cream to soothe the skin and remove traces of foot odor. Alternatively you can opt for creams with rosemary or eucalyptus. You can keep up the foot care by regularly using the pumice stone to tackle cracked heels. Use moisturizers and foot cream to minimize the effect of wear and tear on the feet.

    K-LYINN: UREMBO SIO SURA NA MAUMBILE TU

    Jina lake halisi ni Jacqueline Ntuyabaliwe, nyota yake ni Sagittarius (Mshale). Wengi bado tunamkumbuka kama mrembo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2000 na kisha kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya mrembo wa dunia (Miss World) yaliyofanyikia nchini Uingereza na Visiwa vya Maldives.

    Tofauti na mawazo ya wengi, kama anavyobainisha katika mahojiano tuliyofanya naye hivi karibuni, alianzia kwenye muziki kisha akaja kwenye urembo na baadaye akaamua kurejea katika muziki mahali ambapo ndipo alipo hivi sasa. Mwezi ujao anatarajia kufyatua albamu yake ya pili itakayokwenda kwa jina la K-Lyinn- Crazy Over You.
    Ametoka wapi, nini mtazamo wake kuhusu muziki na urembo, wapenzi wa muziki na mashabiki wake watarajie nini katika albamu yake mpya, nini siri ya urembo wake na anatoa ushauri gani kwa wasichana? Hayo yote na mengineyo ameyaweka bayana katika mahojiano yafuatayo;
    BC: Unaweza kuwaambia mashabiki wako kuhusu maisha yako ya utotoni? Unakumbuka nini kuhusu utoto wako?
    K-LYINN: Utotoni nakumbuka jinsi nilivyokuwa nacheza na baba akirudi kutoka kazini na mara nyingi alikuwa akinipeleka kutembea jioni.Pia nakumbuka nilivyokuwa nikienda kanisani na mama.Nilikuwa napenda sana kusomewa hadithi za vitabu.
    BC: Historia ya maisha yako, kama ilivyoandikwa kwenye tovuti yako, inaonyesha kwamba baada ya shule ulianza shughuli za muziki kwa kuwa mwimbaji wa Tanzanite Band. Baada ya hapo ukaingia kwenye masuala ya ulimbwende ambapo ulifanikiwa kushinda taji la Miss Tanzania mwaka 2000 na kisha baadaye ukarejea kwenye muziki tena. Nini kilivutia kwanza kuingia kwenye muziki na kisha masuala ya ulimbwende?

    K-LYINN:
    Tokea nilipokuwa na miaka sita au saba nakumbuka nilikuwa napenda sana kuiga na kuimba nyimbo za wanamuziki wa ulaya kama Madonna na Mariah Carey,kwahiyo nilipopata nafasi ya kujiunga na bendi ya Tanzanites kwangu ilikuwa kama njia ya kutimiza ndoto yangu.Kuhusu urembo nakumbuka kuna wakati nilikuwa natamani nipate nafasi ya kuvikwa taji na kuwakilisha nchi yangu lakini sana sana niliamua kushiriki baada ya kukutana na watu mbalimbali ambao walinishawishi nishiriki na kunipa moyo kuwa nina nafasi ya kushinda.
    BC: Nini siri ya urembo wako?
    K-LYINN: Kwanza kabisa mimi binafsi napenda sana kujipatia muda mrefu wa kupumzisha akili na viungo kila siku na kupata usingizi wa kutosha na ninaamini hiyo ni siri mojawapo ya urembo.Pia huwa nakunywa maji mengi na kula matunda na mboga katika mlo wa kila siku.Nikipata muda huwa nafanya mazoezi.
    BC: Miaka zaidi ya sita sasa imepita tangu ulipovishwa taji la Miss Tanzania. Unaweza kutukumbusha kidogo ulijisikiaje siku hiyo?
    K-LYINN: Kwanza nilitangazwa kuwa mshindi nakumbuka kuwa nilishikwa na butwaa na ilichukuwa muda kuamini ni mimi niliyeshinda na baada ya kuamini nilijisikia furaha isiyo na kifani.
    BC: Mafanikio uliyoyafikia kwenye masuala ya urembo ni ndoto ya wasichana wengi sana.Je pamoja na muziki bado unajishughulisha na masuala ya urembo? Kama ndio kwa jinsi gani na kama hapana, kwanini umeacha?
    K-LYINN: Kwa sasa huwa sijishirikishi sana na masuala ya urembo kwanza kwasababu kazi ya muziki inachukua muda wangu mwingi,lakini pia ni kwasababu bado hatuna kazi nyingi sana hapa kwetu zinazohusu urembo.
    BC: Unaye mtu yeyote ambaye unamuona kama role model wako? Kwanini?
    K-LYINN: Baba yangu ni role model wangu,ni mtu mkarimu na yeye ni daktari na amejitolea maisha yake kusaidia watu.Pia naamini ni baba mzuri sana kwasababu bahati mbaya mama yangu alifariki miaka kumi na mbili iliyopita na baba alinilea vizuri mpaka nimefikia hapa nilipo.Yeye huwa tayari kunisikiliza muda ninapohitaji kuongea nae na huniunga mkono na kunipa ushauri katika maisha yangu.

    BC: Sasa naomba tuongelee albamu yako mpya unayotarajia kuitoa hivi karibuni.
    Kwanini umeamua kuiita albamu hii K-LYNN?
    K-LYINN: Album yangu inaitwa K-LYINN CRAZY OVER YOU,Nimeamua kuuita hivyo kwasababu napenda watu walifahamu na kulizoea jina langu na Crazy Over You ni jina la single itakayokuwepo katika album yangu.
    You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video
    BC: Je unatunga mashairi ya nyimbo zako zote wewe mwenyewe?
    K-LYINN: Ndio,mashairi yote utakayosikia katika album yangu nimetunga mwenyewe.
    BC: Watu wengi wangependa kufahamu, inakuchukua muda gani kutengeneza albamu nzima kama hii yako?
    K-LYINN: Muda wa kutengeneza album huwa unatofautiana,lakini album hii imenichukuwa mwaka mmoja kuikamilisha.
    BC: Itakuwa na nyimbo ngapi kwa ujumla na imerekodiwa katika studio gani?
    K-LYINN: Album itakuwa na nyimbo kumi,nimefanya kazi na producers tofauti kama Said Comorian,Mwaks,Dunga na Roy.
    BC: Katika albamu hii mpya utakayoitoa hivi karibuni umewashirikisha wasanii gani?
    K-LYINN: Album hii nimemshirikisha Mr.Blu,Sweeza,na Noora.
    BC: Wapenzi wa muziki wategemee nini kipya katika albamu hii?
    K-LYINN: Wapenzi wategemee ujumbe utakaowagusa na mziki utakaowafanya waamke na kucheza.Album hii niliitengeneza kwa ajili ya mashabiki wangu.
    BC: Nyimbo zako nyingi katika albamu iliyopita zilikuwa zinahusu masuala ya mapenzi. Wengi tungependa kujua, kwanini unapenda zaidi kuimba nyimbo za mapenzi? Hadithi zilizoko kwenye mashairi yako zinatokana na uzoefu wako binafsi?

    K-LYINN:
    Napenda kuimba nyimbo tofauti tofauti na lakini kwa sasa naamini nyimbo za mapenzi zinagusa rika tofauti na kuna mambo mengi ya kuimba katika masuala ya mapenzi na zina wapenzi wengi sana,pia katika album hii mpya kuna nyimbo isiyo ya mapenzi.Hadithi zilizoko katika nyimbo zangu zinatokana na hadithi zinazotokea katika maisha ya watu tofauti sio hadithi zangu binafsi.

    BC: Mara nyingi wasanii wa muziki huwa wanakuwa na malengo maalumu katika miziki wanayotunga, kuiimba na hata kucheza. Kwa miaka mingi makundi mawili makubwa yamekuwa ni wale wanaofanya muziki kwa ajili ya kuelimisha na wanaofanya kwa ajili ya kuburudisha. Muziki wako upo zaidi katika kundi gani kati ya haya?
    K-LYINN: Nafanya muziki kwa ajili ya kuburudisha na kuelimisha kwa ujumla.
    BC: Nini maoni yako kuhusu muziki wa kizazi kipya ambapo katika siku za hivi karibuni umekuwa ukizungumziwa kama muziki utakaopita haraka kutokana na kukosa ujumbe wa maana?
    K-LYINN: Mimi naamini mziki wa bongo flavour unaweza kufananishwa na mziki wa R&B na mziki usioweza kupita kwani aina ya mziki huu hubadilika kutokana na wakati,si kweli kwamba mziki huu hauna ujumbe kwasababu ziko nyimbo nyingi sana ambazo zina mashairi yenye ujumbe wa maana ila labda mwelekeo wa sasa asilimia kubwa ni nyimbo za mapenzi kwasababu inaonekana kuwa zina wapenzi wengi lakini msanii mwenye kipaji anaweza kubadilika na kutunga mashairi yenye maudhui tofauti inapohitajika.
    BC: Ukiacha wewe mwenyewe, ni msanii au wasanii gani duniani wanaokuvutia sana na ambao ungependa kufanya nao kazi siku za mbeleni?

    K-LYINN:
    Namzimia sana Beyonce na Mary J Blige,kwa wasanii wa kiume ningependa
    kufanya kazi na Usher Raymond,Neyo,Basta Rymes na Jay Z.
    BC: Mbali ya Tanzania umewahi kufanya perfomances katika nchi gani zingine? Huwa unajisikiaje kuperfom nje ya Tanzania?
    K-LYINN: Nimeshawahi kufanya performances nje na bendi,na kwa ajili ya kuitangaza album yangu ninapanga kufanya tour katika baadhi ya nchi za Africa na UK na US pamoja na baadhi ya nchi za Europe.Ratiba za shows zitapatikana katika website yangu www.klyinn.com
    BC: Unatoa ushauri gani kwa wasichana wadogo wanaotaka aidha kuingia kwenye mambo ya urembo au muziki? Nini tofauti kati ya fani ya muziki na urembo?
    K-LYINN: Wasichana wanaopenda kuingia katika masuala ya urembo nawaambia kuwa kwanza wasome na wasubiri kufikia umri unaotakiwa,urembo sio sura na maumbile tu bali pia ni ufahamu na mambo mengi mengine huwa yanayotakiwa.Na ili kufanya muziki ni muhimu kuwa na kipaji asilia na kama wanaweza kusomea fani hiyo wataweza kufanikiwa zaidi kwani muziki ni kama biashara ambayo kama unaifanya vizuri unaweza kuitumia kuendesha maisha.
    BC: Kwa wapenzi wa muziki ambao wangependa kununua albamu yako unawaambia nini? Nani msambazaji wako na itapatikana katika maduka gani?
    K-LYINN: Wapenzi wa muziki wangu watakaopenda kununua album yangu napanda kuwaambia kuwa album yangu ikishatoka watapata taarifa za mahali au maduka zitakapokuwa zikiuzwa katika matangazo na vile vile katika website yangu WWW.KLYINN.COM.
    BC: Asante K-Lyinn kwa mahojiano haya na kila la kheri.
    K-LYINN: Asanteni pia.

    Madawa ya kulevya katika Mombasa


    Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
    Rukia: urambazaji, tafuta
    Utumiaji wa madawa ya kulevya imekuwa mojawapo ya masuala makubwa nchini Kenya hasa katika Mombasa ambayo ni sehemu zilizoathirika zaidi ya nchi. Wakazi wengi hasa wanaume wameadhiriwa na suala hili.La kuhatarisha sana ni kuwa wengi wanaotumia madawa haya wako katika unri wa ishirini .Akina mama mjini Mombasa wamefanya maandamano wakitaka serikali kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya miongoni mwa vijana katika eneo hili.Katika Kilindini mjini Mombasa kuna maeneo arobaini ambayo walevi hutambua kama ' maskani' ambapo wao hukutana ilikutumia madawa haya.Hivi sasa Utumiaji wa heroin umepita wa bangi .Asilimia sabini wanaotumia madawa ya kulevya wamekiri kuwa wao hutumia heroine.

    Yaliyomo

    [ficha]

    [hariri] Sababu za Kuongezeka kwa utumiaji wa madawa ya kulevya

    [hariri] Ukosefu wa ajira

    Nchini Kenya kiwango cha ukosefu wa ajira kimo juu sana.Ukosefu wa ajira umesababisha vijana wengi kukaa ovyo bila chochote ca kufanya na kugeukia madawa ya kulevya.

    [hariri] shinikizo kutokana na marafiki.

    Hii ni moja ya sababu kuu ya kutumia madawa ya kulevya. Wengi wanaotumia madawa ya kulevya katika ukanda huu wamekubali kwamba walianza kutumia madawa kwa sababu wengi marafiki wao walikuwa wanatumia .Wengi wa mavijana ambao wanapatikana kule baharini wanatumia madawa haya ili wapate ujasiri wa kuzungumza na wateja wao.

    [hariri] Ushirikina

    Wakazi wengi wa eneo hili wanaamini ushirikina. Kulingana na utafiti uliofanywa nchini hivi juzi inaaminika kuwa vijana wengi katika mkoa huu unatumia madawa wanafanya hivi kwa sababu ya kujihami kutyokana na uvamizi wavizuka.

    [hariri] Athari

    [hariri] Uhalifu

    Katika ukanda huu vijana hawa hawawezi kukaa bila kutumia dawa hizi. Dawa hizi huwa ghali mno na la kusikitisha ni kuwa vijana hawa hawana ajira. Hiii inamaanisha kuwa vile wanavyoweza kupata pesa ni kwa kuwaibia wakazi wenzao. Hii inasababisha usalama wa ukanda huu kutoaminika.

    [hariri] Maradhi

    Hii ni athari kubwa ya madawa ya kulevya. Kuna maradhi mengi ambayo vijana hawa wanapata kutokana na madawa haya. Baadhi yao wamekuwa wamukuwa wendawazimu. Maradhi haya yanawapata vijana hawa kwa kasi mno kwa sababu ya kutokula vyema.Hawa vijana hawali lakini wanaendelea kutumia madawa haya.Pia wanaambukizana maradhi kwa kubadilishana sindano. Hii imesababisha kusambaa kwa UKIMWI katika eneo hili.

    [hariri] Kukosekana kwa maendeleo

    Madawa ya kulevya pia yamesababisha kutoendelea katika eneo nyingi za Mombasa ambayo ndiyo bandari kubwa katika Afrika Mashariki. Hii ni kutokana na uhaba unaosababishwa na baadhi ya wanaotumia madawa ya kulevya ambao huwashambulia wakazi wa eneo hizi.Jambo hili hutisha wanabiasharana kuwafanya wahamie mbali na eneo hizi.Vijana hawa pia huwa wavivu na hawataki kufanya jambo lolote ambalo laweza kusaidia kukuza eneo hizi,wao wanataka kuketi na kuvuta bangi.

    [hariri] Kifo

    Mwishowe adhari hizi zote zaelekeza kaburini. Kiwango cha kifo katika ukanda huu kinaongezeka kwa kasi mno. Vijana wengi katika ukanda huu wanaaga dunia katika miaka yao ya thelathini.Vifo hivi vinasababishwa hasa na maradhi yanayoletwa na madawa ya kulevya. Hili ni jambo linatia nchi ya Kenya wasiwasi kwani vijana wengi waaga katika ukanda huu.

    [hariri] Marejeleo

    Elimu, Kazi na Fedha

     
    Ujuzi ni nguvu na Elimu ni ufunguo wa maisha. Watu huenda shule ili waweze kupata elimu na ujuzi kwa ajili ya ajira itakayowapatia fedha. Unahitaji kuwa na elimu nzuri ili kupata kazi nzuri. Kwa ajili ya mbinu za kuchagua shule nzuri, kujenga taaluma, kupata kazi nzuri, kuandika wasifu wako, kujiandaa kwa usaili kwa ajili ya kazi na utunzaji mzuri wa fedha zako, Elimika na kipengele hiki.


    Plani taaluma yakoPlani taaluma yako
    Umemaliza shule? Nini mipango yako ya baadaye? Amua na upangilie taaluma yako leo. Pata mbinu za kupanga taaluma hiyo hapa!


    Kutafuta kazi Kutafuta kazi
    Cheki mbinu zitakazo kuwezesha kuandika wasifu wako (CV), jinsi ya kuomba kazi na kujiandaa kwa usaili. Bofya hapa


    Utunzaji wa fedhaUtunzaji wa fedha
    Pata mbinu za utunzaji wa fedha na jinsi ya kufanya manunuzi yako kwa busara.


    ZaidiZaidi
    Pata habari zaidi kuhusu elimu, kazi na masuala ya fedha hapa!


    Stori yanguStori yangu
    Sikiliza habari za kweli kutoka kwa watu wakweli kuhusiana na kazi zao, matatizo na mafanikio. Uzoefu wao waweza kukujenga! Usipuuzie soma stori hizo hapa!

    Urafiki, Mapenzi na Ndoa

     
    Hivi maisha yangekuwa vipi kama kusingekuwepo na urafiki? Rafiki si mtu tunayecheka na kufurahia naye maisha tu bali pia tunayekuwa naye katika shida na raha! Marafiki hutusaidia kupata majibu ya maswali mbalimbali yanayotukabili. Katika ndoa, Urafiki ni msingi imara kwani Wanandoa wanatakiwa kuwa marafiki. Lakini, rafiki wa kweli ni nani? Anatakiwa kuwa na sifa gani? Mjue rafiki longolongo hapa.


    MichapoMichapo
    Stori za kweli za watu, zisome ujipatie uzoefu


    ZaidiZaidi
    Kuna mengi zaidi ya kufahamu kuhusiana na masuala haya...


    Maswali na MajibuMaswali na Majibu
    Hapa unaweza kupata majibu ya maswali yaliulizwayo kila mara kuhusu urafiki, mapenzi na ndoa

    Madawa ya kulevya

     
    Wote tunapenda kujisikia vizuri! Tunataka kujisikia kuwa na raha, wenye nguvu na siyo wasiwasi. Hivyo tunaweza tukifikiri kuwa dawa za kulevya, pombe na sigara zitatupa hali hizo. Chunga sana! Usijidanganye! Kutumia vitu hivyo ili kupata furaha ni hatari kwani unaweza kujikuta umetopea ulevini! Kujinasua kutoka kwenye hali hiyo si lelemama! Inahitaji moyo na kujizatiti kweli kweli! Jua athari za dawa za kulevya na wapi pa kwenda kwa msaada ili ubadilike hapa.


    Aina za MadawaAina za Madawa
    Fahamu aina ya dawa za kulevya zitumiwazo zaidi nchini.


    AthariAthari
    Dawa hizi hudhuru akili na mwili na husababisha mtumiaji kuzitegemea. Huleta matatizo ya kisaikolojia, kijamii, ugumba nk. Zifahamu ili ukae mbali nazo!


    ZaidiZaidi
    Mambo mengine mengi tu ya kufahamu kuhusu dawa za kulevya


    Niende wapi Niende wapi
    Sehemu ambazo unaweza kwenda kupata msaada ikiwa umeathirika au unamfahamu aliyeathirika na dawa za kulevya zimeorodheshwa.


    Maswali na MajibuMaswali na Majibu
    Pata majibu ya maswali yaulizwayo kila mara kuhusiana na dawa za kulevya na athari zake hapa.


    Stori yanguStori yangu
    Sikiliza habari za kweli kutoka kwa watu waliotumia dawa za kulevya, walivyoathirika na walivyobadilika.

    Ujumbe wa simu wazua hofu


     Send to a friend



    Richard Kihiyo
    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watumiaji wa simu za mikononi kupuuza ujumbe wa tahadhari ulioanza kusambazwa jana na watu wasiojulikana, ikisema kuwa ni uzushi.
    Jana kulikuwa na aina mbili za taarifa za tahadhari zilizokuwa zikitumwa kwa wateja wa simu za mikononi. Ujumbe wa kwanza unasema: “Ukipigiwa simu kwa private no (namba binafsi). au ikiandika call kwa red colour (rangi nyekundu) usipokee, ni mionzi, utapalarize (utapooza) na kufa.
    Imetokea Kenya watu wamekufa. Julisha ndugu na jamaa wote.” Ujumbe mwingine unawataka watumiaji wa huduma hiyo wasipokee simu yoyote watakayopigiwa kupitia namba 7888308001, 9316048121, 9876266211, 9888854137 na 9876715587.
    Ujumbe huo unasema: "Namba hii inapigwa na rangi nyekundu, unaweza kupata brain damage (tatizo la ubongo) kwa kupokea simu.
    Watu 27 walifariki mara tuu baada ya kupokea simu iliyopigwa kutoka katika namba hizo." Ujumbe huo ulisababisha watumiaji wa simu kuingiwa na wasiwasi na baadhi waliwasiliana na chumba cha habari cha Mwananchi Communications kutaka ufafanuzi wa suala hilo na wengine wakieleza hofu ya kupooza.
    Hata hivyo, taarifa iliyotumwa na msemaji wa TCRA, Innocent Mungy ambayo imesainiwa na kurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkhoma, inasema: “Ujumbe huo unatakiwa kupuuzwa kwa kuwa ni uzushi usuokuwa na ukweli wowote.” Kutokana na ujumbe huo kusambazwa kwa watu wengi, TCRA imesema hakuna ukweli na hivyo kuwataka wananchi kuupuuzia. "Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli.
    Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote," inasema taarifa hiyo ya TCRA.
    Ilifafanua kuwa kutokanha na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu mbalimbali duniani ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. 
    TCRA iliwataka wote kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta ambazo zinatumiwa ulimwenguni kote bila madhara yoyote. "Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema," inasema sheemu ya taarifa hiyo.
    Mmoja wa watumiaji wa simu za mkononi, Frank Kimboyi ambaye naye alitumiwa ujumbe huo, alisema mwanzoni alipata wasiwasi mkubwa. "Baada ya kuupokea kidogo nilishituka, lakini baada ya kukaa na kutafakari uwezekano wa kitu kama hicho kutokea niliona ni mdogo na nikaamua kuupuuzia," alisema Kimboyi.