Saturday, September 4, 2010

Madawa ya kulevya katika Mombasa


Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Utumiaji wa madawa ya kulevya imekuwa mojawapo ya masuala makubwa nchini Kenya hasa katika Mombasa ambayo ni sehemu zilizoathirika zaidi ya nchi. Wakazi wengi hasa wanaume wameadhiriwa na suala hili.La kuhatarisha sana ni kuwa wengi wanaotumia madawa haya wako katika unri wa ishirini .Akina mama mjini Mombasa wamefanya maandamano wakitaka serikali kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya miongoni mwa vijana katika eneo hili.Katika Kilindini mjini Mombasa kuna maeneo arobaini ambayo walevi hutambua kama ' maskani' ambapo wao hukutana ilikutumia madawa haya.Hivi sasa Utumiaji wa heroin umepita wa bangi .Asilimia sabini wanaotumia madawa ya kulevya wamekiri kuwa wao hutumia heroine.

Yaliyomo

[ficha]

[hariri] Sababu za Kuongezeka kwa utumiaji wa madawa ya kulevya

[hariri] Ukosefu wa ajira

Nchini Kenya kiwango cha ukosefu wa ajira kimo juu sana.Ukosefu wa ajira umesababisha vijana wengi kukaa ovyo bila chochote ca kufanya na kugeukia madawa ya kulevya.

[hariri] shinikizo kutokana na marafiki.

Hii ni moja ya sababu kuu ya kutumia madawa ya kulevya. Wengi wanaotumia madawa ya kulevya katika ukanda huu wamekubali kwamba walianza kutumia madawa kwa sababu wengi marafiki wao walikuwa wanatumia .Wengi wa mavijana ambao wanapatikana kule baharini wanatumia madawa haya ili wapate ujasiri wa kuzungumza na wateja wao.

[hariri] Ushirikina

Wakazi wengi wa eneo hili wanaamini ushirikina. Kulingana na utafiti uliofanywa nchini hivi juzi inaaminika kuwa vijana wengi katika mkoa huu unatumia madawa wanafanya hivi kwa sababu ya kujihami kutyokana na uvamizi wavizuka.

[hariri] Athari

[hariri] Uhalifu

Katika ukanda huu vijana hawa hawawezi kukaa bila kutumia dawa hizi. Dawa hizi huwa ghali mno na la kusikitisha ni kuwa vijana hawa hawana ajira. Hiii inamaanisha kuwa vile wanavyoweza kupata pesa ni kwa kuwaibia wakazi wenzao. Hii inasababisha usalama wa ukanda huu kutoaminika.

[hariri] Maradhi

Hii ni athari kubwa ya madawa ya kulevya. Kuna maradhi mengi ambayo vijana hawa wanapata kutokana na madawa haya. Baadhi yao wamekuwa wamukuwa wendawazimu. Maradhi haya yanawapata vijana hawa kwa kasi mno kwa sababu ya kutokula vyema.Hawa vijana hawali lakini wanaendelea kutumia madawa haya.Pia wanaambukizana maradhi kwa kubadilishana sindano. Hii imesababisha kusambaa kwa UKIMWI katika eneo hili.

[hariri] Kukosekana kwa maendeleo

Madawa ya kulevya pia yamesababisha kutoendelea katika eneo nyingi za Mombasa ambayo ndiyo bandari kubwa katika Afrika Mashariki. Hii ni kutokana na uhaba unaosababishwa na baadhi ya wanaotumia madawa ya kulevya ambao huwashambulia wakazi wa eneo hizi.Jambo hili hutisha wanabiasharana kuwafanya wahamie mbali na eneo hizi.Vijana hawa pia huwa wavivu na hawataki kufanya jambo lolote ambalo laweza kusaidia kukuza eneo hizi,wao wanataka kuketi na kuvuta bangi.

[hariri] Kifo

Mwishowe adhari hizi zote zaelekeza kaburini. Kiwango cha kifo katika ukanda huu kinaongezeka kwa kasi mno. Vijana wengi katika ukanda huu wanaaga dunia katika miaka yao ya thelathini.Vifo hivi vinasababishwa hasa na maradhi yanayoletwa na madawa ya kulevya. Hili ni jambo linatia nchi ya Kenya wasiwasi kwani vijana wengi waaga katika ukanda huu.

[hariri] Marejeleo

No comments:

Post a Comment